Terms of Service

Masharti haya yanaongoza matumizi ya Lastborn eFootball Store.

Kukubali masharti

Kwa kutumia Lastborn eFootball Store unakubali masharti haya. Kama hukubaliani nayo, tafadhali usitumie huduma hii.

Akaunti

Lazima ujisajili kwa email na password ili kununua kikosi, kununua vifaa vya game au kujiunga na chanel. Wewe ndiye mwenye jukumu la usalama wa akaunti yako.

Manunuzi na malipo

Malipo yote hufanyika kupitia namba tunazokupa kwenye ukurasa wa malipo au WhatsApp. Bidhaa hukabidhiwa baada ya malipo kuthibitishwa. Hatuwajibiki kwa malipo yaliyotumwa kwa namba ambazo hazikutolewa nasi rasmi.

Uuzaji wa vikosi

Unapouza kikosi lazima utoe picha na video zinazoonesha account yako yote ndani ya muda uliopangwa. Taarifa za uongo au udanganyifu husababisha akaunti kufungiwa.

Matumizi yasiyoruhusiwa

Ni marufuku kutumia mfumo huu kwa utapeli, kutuma maudhui ya matusi, au kujaribu kuingilia mfumo. Tunaweza kuzuia akaunti yoyote inayovunja masharti haya bila taarifa ya awali.

Mabadiliko ya masharti

Tunaweza kubadilisha masharti haya wakati wowote. Matumizi yako ya huduma baada ya mabadiliko yanamaanisha umekubali masharti mapya.

Mawasiliano

Kwa maswali kuhusu masharti haya, wasiliana nasi kupitia WhatsApp namba +255 699 276 287.